-Awakaribisha wageni kutoka nchi zaidi ya 13 washiriki wa Mkutano huo, asema DSM ni Safi na Salama
- Amesema matumizi ya umeme badala ya mafuta kwenye vyombo vya usafiri yana faida kubwa
-Asema Rais Dkt Samia amepanga kujenga Dar ya mwendokasi miradi 6 Serikali imetenga zaidi ya Trilioni 2 kujenga miundo mbinu ya Mwendokasi (DART)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla leo Machi 21, 2023 amefungua mkutano mkubwa maarufu kwa jina la " *Africa E-Mobility Forum* " unaozihusisha nchi zaidi ya 13 katika Ukumbi wa Hotels ya Hyatt Regency
CPA Makalla akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa OR- TAMISEMI Mhe Angelah Kairuki amesema mradi wa kutumia nishati ya Umeme badala ya mafuta kwenye vyombo vya usafiri unafaida nyingi ikiwemo kupunguza uchafuzi wa hewa, Kupunguza gharama, na kupunguza athari za mabadiliko ya hali hewa
Aidha CPA Amos Makalla amebainisha mradi wa kutumia Umeme kwenye vyombo vya usafiri (motor vehicles) umekuja muda muafaka ambapo Rais Dkt Samia amepanga kujenga Dar ya mwendokasi ambapo miradi 6 imetengewa pesa zaidi ya trilioni 2 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, hivyo DART watakua tayari kupokea mabadiliko hayo ya matumizi ya umeme kwa masilahi mapana ya Umma
Mwisho CPA Amos Makalla amewakaribisha wegeni kutoka nchi zaidi ya 13* kuifurahia Tanzania wakati wote wa mkutano huo hususani Jiji la Dar es Salaam ambalo linakua kwa kasi (Fast Growing City) ni Salama, Safi pia lina vivutio vingi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa