- Asema ni mwarobaini wa utekelezaji wa miradi inayokwama kwa kukosa bajeti
- Asisitiza Viongozi katika ngazi za Wilaya kuwa na uelewa wa Hati fungani.
- Asema anataka Mkoa wa Dar es Salaam uwe chuo kwa Mikoa mingine kujifunza Hati fungani
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Septemba 8, 2021 amefungua kikao kazi cha Siku 3 cha mafunzo ya Hati Fungani kwa Serikali za Mitaa katika Ukumbi wa Anatoglo Ilala Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Wataalam Kutoka TAMISEMI yenye lengo la kuwapa mafunzo Viongozi wa ngazi za Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam hususani Sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu tawala wa Wilaya, Wakurugenzi na Wataalam wengine.
Akiongea wakati wa ufunguzi Mhe Makalla amewashukuru TAMISEMI kwa kuandaa mafunzo hayo kwa kuwa ndio utakuwa mwarobaini wa kutekeleza miradi ya Kimkakati katika Halmashauri ambayo ilikuwa inakwama kutokana na ufinyu wa bajeti.
" Kupitia Hati fungani miradi ya maendeleo katika Wilaya hususani ile ya Kimkakati itafadhiliwa, ni imani yangu kuwa Dar es Salaam itakuwa Pilot area" Alisema Mhe Makalla
Aidha Mtaalamu kutoka TAMISEMI Ndg John Cheyo amefafanua kuwa Hati fungani kwa Serikali za Mitaa ni mpya lakini ilikuwa inatekelezwa sana Serikali Kuu kwa kutambua umuhimu wake imeonekana kuna kila sababu ya Kuwa na Hati fungani kwa Serikali za Mitaa.
Kwa kuwa katika Serikali za Mitaa kuna miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa na wakati mwingine inakwama kwa kukosa fedha hivyo kupitia Hati fungani miradi hiyo itafadhiliwa, kitakachohitajika katika mradi husika ni kufanyika kwa upembuzi yakinifu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa