- Aelekeza vijana hao kuripoti katika Wilaya za Mkoa wa DSM wapatiwe majukumu ya Ulinzi Katika MITAA na KATA
- Aahidi kupeleka maombi katika mamlaka husika ili waliohitimu mgambo iwe moja ya sifa ya kupata ajira Jeshini
- Ataka Vijana Kushirikiana na Jamii katika Ulinzi na Usalama
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo Novemba 5, 2021 amefunga Mafunzo ya kuhitimu kwa Askari 628 wa Jeshi la Akiba mkoani humo na kutoa wito kwa Vijana hao wa Mgambo kujituma kufanya kazi kwa bidii na weledi pia kuwa Viherehere wa kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini viashiria vya uhalifu ili Kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya Mkoa
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mhe Makalla amewaelekeza Wahitimu hao kufika ofisi za *Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ili wapangiwe shughuli za ulinzi kwenye kila ofisi za Mtendaji wa Mitaa ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo aliyotoa ya kila Ofisi ya Mtaa kuwa na Askari Mgambo Kufuatia kuuwawa kwa Mtendaji wa Mitaa wa Msumi.
Aidha Mhe Makalla ametoa wito kwa Vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza kipengele Cha kuhitimu wa Mafunzo ya Mgambo kuwa moja ya sifa za kujiunga na Jeshi la Polisi, Uhamihaji, Zimamoto na Magereza tofauti na Sasa ambapo kigezo Ni kupitia mafunzo ya JKT pekee.
Katika Mafunzo ya hayo, Askari Mgambo wamepata elimu mbalimbali ikiwemo Ukakamavu, Mbinu za kivita, Zimamoto, Uhamihaji, TAKUKURU, Usalama wa Taifa na mbinu nyinginezo za Kudhibiti uhalifu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa