-Asema Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe Angellah Kairuki anawapongeza kwa Moyo, Uzalendo na mchango wa NDC kwa Taifa
-Ahadi ya Mhe Waziri Kairuki Serikali itaendelea kuwaleta Viongozi wengi zaidi kupata mafunzo NDC
- RC Makalla awataka Viongozi waliopata mafunzo kutumia katika kutatua migogoro ya wananchi
CPA Amos Makalla kulia akiwa katika picha na Mkuu wa Chuo NDC Meja Jenerali Michael Mhona baada ya kuwasili chuoni hapo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla leo Februari 10, 2023 amefunga mafunzo ya 14 katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) yaliyohusisha Viongozi wa mhimili wa Dola, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala, Wakurugenzi, na Viongozi waandamizi kutoka kwenye Wizara
CPA Makalla wakati akifunga mafunzo hayo amesema amekuja kwa niaba ya Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe Angellah Kairuki ambaye ameshindwa kuja kutokana na sababu zisizo zuilika, ambapo amesema Mhe Waziri anakipongeza NDC kwa Moyo, Uzalendo, na mchango wake kwa Taifa katika kutoa mafunzo Usalama wa Taifa na Stratejia kwa Viongozi mbalimbali hapa nchini.
Aidha CPA Makalla amebainisha katika hotuba ya Waziri wa OR-TAMISEMI ahadi yake ni kuwa Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na chuo hicho kwa kuleta Viongozi wengi zaidi kwa masilahi mapana ya Taifa
Hata hivyo CPA Makalla amewataka Viongozi waliopata mafunzo katika chuo hicho kutumia maarifa waliyopewa *kutatua migogoro ya wananchi katika maeneo yao*, wananchi wanachanga moto nyingi na wanaimani kubwa na Viongozi hususani wateule wa Rais.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenelari Ibrahim Michael Mhona amesema mafunzo waliyopatiwa Viongozi takribani 114 yakiongozwa na kauli Mbiu " Uongozi wa Kimkakati kwa Mazingira Yanayobadika kiusalama Tanzania" wameyapata kwa asilimia mia moja, malengo ya kozi yamefikiwa wajibu wao ni kwenda kuyafanyia kazi yale waliyojifunza kwa muda wa siku 5 kwa lengo la kuleta Ustawi wa Jamii na Taifa kwa Ujumla.
Mafunzo hayo ni ya 14 ambapo wahitimu wapatao 114 wamehitimu, ni mafunzo ya muda mfupi ambayo Viongozi wameyapata kwa siku 5 kuanzia Februari 06, 2023 hadi leo ebruari 10,2023 katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania- Kunduchi Wilaya ya Kinondoni
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa