- Amaliza Mgogoro wa Ardhi uliodumu kwa muda mrefu Boko Dovya kwa Somji- Kinondoni
- Atoa punguzo kwa Wakazi wa eneo hilo kuchangia Tsh 8,000/= kwa square mita moja badala ya Tsh 30,000/= bei ya Soko kwa sasa
- Wananchi wa mshukuru , Aelekeza Manispaa ya Kinondoni kuanza Mara moja mchakato wa upimaji na atakaye kamilisha apatiwe HATI yake
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla amemaliza Mgogoro wa Ardhi uliodumu kwa muda mrefu katika eneo la Boko Dovya kwa Somji -Kinondoni, Dar es Salaam
RC Makalla ametatua Mgogoro huo kwa njia shirikishi ambapo awali alizuru katika eneo hilo kujionea na kuwa na Mkutano na Wananchi kusikiliza mapendekezo yao, akiwapa fursa ya kuongea mmoja mmoja.
Baadaye akamkaribisha kamishna wa Ardhi Mhandisi Idrisa Kayera kutoa utaratibu wa Kitaalam wa gharama za upimaji wa Ardhi katika eneo hilo ambapo mtaalam anasema gharama ya mbweni Square mita moja kwa sasa ni Tsh 50,000/= hadi 80,000/= na Boko Bunju ni Tsh 25,000 hadi 35,000/= na gharama hizo zinatofautiana kutokana thamani ya eneo husika
Kwa Upande wa mtaalam wa Ardhi Manispaa ya Kinondoni wamesema wao wanatambua Gharama halisi za eneo hilo Kitaalam kama alivyosema Kamishna wa Ardhi lakini kwa kutambua gharama za Maisha kwa sasa wametoa pendekezo la mwananchi kuchangia Tsh10,000/= kwa Square mita moja ili aweze kupimiwa na kupatiwa Hati ya Ardhi
Aidha RC Makalla akatoa tamko la busara kwa kusema anawapunguzia Zaidi hadi Tsh 8,000 kwa Square mita ili wananchi hao waweze kuchangia na kuwataka wataalam kuanza mchakato huo mara moja na atakaye kamilisha apatiwe HATI yake.
Wananchi wamemshukuru RC Makalla na wamepongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chini ya Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali Wananchi
Ifahamike kuwa eneo la Dovya Kwa Somji lina ukubwa wa Square mita Milioni 1.4 ikiwa Serikali imetenga zaidi ya Square mita laki 2 kwa ajili ya huduma za Kijamii na Square mita zilizobaki ni kwa ajili ya makazi ya wananchi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa