-Ataja mafanikio lukuki yaliyofanyika DSM katika nyanja mbalimbali
- Asema Rais Dkt Samia Suluhu ni kiongozi mahiri na shupavu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla leo Machi 8, 2023 ameeleza mafanikio ya Utekelezaji wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu kwa Kipindi cha miaka miwili 2021/2022- 2022/2023
CPA Makalla ameeleza mafanikio hayo katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na Viongozi wa Chama na Serikali, pia Wadau wa maendeleo katika Mkoa huo.
Akiongea mbele ya hadhara hiyo CPA Amos Makalla ametaja mafanikio lukuki yaliyofanyika katika kipindi cha miaka miwili ndani ya Mkoa huo akiangazia katika nyanja mbalimbali kama Ulinzi na Usalama, Ukusanyaji wa mapato TRA na Halmashauri, Utoaji huduma za Afya, Elimu na Mafunzo, Utoaji huduma za maji, Nishati, Uwezeshaji wanawake kiuchumi, Kuwapanga vizuri wamachinga na uboreshaji wa miundombinu, kurasimisha bodaboda, Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DSM, Bandari, Reli ya Kisasa, miradi ya DMDP, TARURA, Miundombinu ya mabasi yaendayo kasi DART na miradi ya Kimkakati ikiwemo Soko la karikaoo, Kisutu Magomeni na Kituo cha mabasi Magufuli
Aidha *CPA Makalla* amefafanua miradi yote ya kisekta *imetekelezwa kwa ufanisi mkubwa* katika Kipindi cha miaka miwili toka Mhe Rais *Dkt Samia* aingie madarakani
Mwisho Mkoa wa DSM unampongeza *Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi wake mahiri na mafanikio makubwa* aliyoyaleta katika Mkoa na Taifa kwa Ujumla, jukumu la Serikali ya Mkoa ni kuendelea *kuimarisha Ulinzi na Usalama, Ukusanyaji wa mapato,matumizi sahihi ya rasilimali za Umma* na *Utekelezaji wa miradi ya maendeleo*, KAZI UENDELEE
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa