- Ni hatua za kukabiliana na Changamoto ya ufinyu wa eneo.
- Shule ya Msingi pekee Ina Wanafunzi 4,515 na eneo la Ujenzi wa madarasa ni finyu.
- Aelekeza Maeneo ya Shule kupimwa na kuwekewa mipaka/ uzio ili kukabiliana na Wavamizi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla ametoa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya Temeke kupitia kitengo Cha Uhandisi kukamilisha michoro ya Ujenzi wa madarasa ya gorofa Shule ya Msingi Buza ili kukabiliana changamoto ya ufinyu wa eneo.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara Shuleni hapo na kujionea changamoto mbalimbali ikiwemo Uhaba wa Matundu 100 ya Vyoo, upungufu wa Madarasa 62 na Madawati 657.
Upungufu huo umetokana na Shule kuwa na idadi kubwa ya Wanafunzi Kutokana na uamuzi wa Serikali kufuta ada kuanzia Msingi mpaka kidato Cha sita mbapo Shule ya Msingi Buza pekee Ina jumla ya Wanafunzi 4,515.
Aidha RC Makalla ameelekeza Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha Maeneo ya Shule yanapimwa na kuwekewa mipaka/uzio ili kutatua changamoto ya uvamizi wa maeneo ya Shule.
Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza maeneo yaliyotengwa kwaajili ya Viwanja vya Michezo yabaki kwa Matumizi hayohayo na sio Ujenzi wa madarasa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa