RC Makalla amepokea taarifa ya mikopo ya asilimia kumi 10% Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Mkutano uliowajumuisha Viongozi na Watendaji wa Mkoa wakiwemo Sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Mameya, wataalam wa maendeleo ya Jamii, waweka Hazina na wadau mbalimbali kutoka katika majukwaa ya Kuwezesha Wananchi Kiuchumi katika Ukumbi wa Arnatoglo Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam
Baada ya kupokea taarifa hiyo ambayo imeonyesha zaidi ya Bilioni 13.2 zimetolewa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021. Mhe Makalla alipata wasaa wa kusikia maoni na mawazo kutoka kwa wadau ambao ni wanufaika kama vile makundi maalum ya watu wenye ulemavu, Viongozi wa majukwaa, na muasisi wa VICOBA Bi Devotha Likokola
Aidha RC Makalla ameagiza kufanyika kwa mambo yafuatayo katika Wilaya zote za DSM.
- Mikopo iendelee kutolewa ni takwa la kisheria Mkuu wa Mkoa ameelekeza kuwa Mikopo ya 10% sio hisani ni takwa la kisheria hivyo kila Manispaa ni lazima watekeleze takwa hilo.
- Kufanyika kwa vikao na wadau wa mikopo mara 4 kwa mwaka katika vikao hivyo washirikishwe wadau wote muhimu kama majukwaa anuai ya wanawake, na vikundi vya VICOBA kwa Upande wa Mkoa kwa mwaka vikao vitafanyika mara 2.
- Mafunzo ya masuala ya Fedha wanufaika wa mikopo wapatiwe mafunzo ya masuala ya fedha ili waweze kukopa na kurejesha, kama ni mzalishaji wa bidhaa afundishe namna bora ya kuifanya bidhaa yake iwe na ushindani sokoni.
- Maonyesho ya wanufaika wa mikopo Kila Wilaya iandae Maonyesho ambayo yatatoa ushaidi mzuri kwa mnufaika ili watu wengine waone.
- Maeneo ya kufanyia biashara Kila Wilaya kuwe na maeneo rafiki ya kuwawezesha wanufaika wa mikopo kufanya biashara yenye kuleta tija.
- Mamlaka za Udhibiti biashara* kama TBS na nyinginezo zisiwe kikwazo kwa wafanyabishara ambao ni wanufaika wa mikopo zisiwakatishe taamaa badala yake ziwatie moyo.
- Masoko Wanufaika wa mikopo wakiwa na masoko ya uhakika itasaidia kuwa na uwezo wa kurejesha mikopo yao na namna mojawapo ya kupata masoko ni kuzalisha katika viwango vinavyokidhi ushindani katika Soko hivyo ni jukumu la wataalam kutoa elimu hiyo.
- Majukwaa ya wanawake DSM yafufuliwe maazimio ya kikao majukwaa ya wanawake ambayo yalilenga kuwawezesha Kiuchumi yafufuliwe kwa kuwa ndio sehemu ya wanawake kukutana kujadili biashara na Uchumi.
- Marejesho ya Mikopo RC Makalla amesema mikopo hiyo inatolewa kwa kikundi kwa masharti afanye biashara arejeshe na akopeshwe mwingine hivyo Maafisa maendeleo ya jamii katika kila Wilaya wakasimamie hilo.
Mwisho RC Makalla amesema Rais Samia Suluhu amekuwa akitilia mkazo suala la kuwezesha Kiuchumi makundi maalum, wanawake, na vijana hivyo yeye kama msaidizi wake DSM yuko tayari kutekeleza hilo kwa umakini na weledi mkubwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa