- Achoshwa na "Danadana" za kila siku.
- Asema ziara za Rais Samia Suluhu Hassan nje ya Nchi zimefungua Fursa ya Biashara ya Nyama.
- Ataka Mkandarasi kusimamiwa kikamilifu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kumsimamia kikamilifu Mkandarasi anaefanya Ujenzi wa chumba Cha kuhifadhi Nyama (Cold room) na Mabucha ya Nyama kwa kuhakikisha kazi inafanyika usiku na mchana ili ifikapo August 30 Mwaka huu machinjioni iwe imekamilika.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipofanya ziara kwenye machinjio hiyo ambayo Ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 15.4 na Sasa Mradi umefikia Asilimia 97.
Aidha RC Makalla amesema Ziara za Rais Samia Suluhu Hassan nje ya Nchi zimefungua Fursa ya Biashara ya Nyama hivyo ni lazima machinjio ikamilike kwa mustakabali wa Soko la Nyama nje ya Nchi.
Hata hivyo RC Makalla amewataka Wafanyabiashara wa Nyama kwenye machinjio hiyo kubadilika kwa kufuata utaratibu watakaopewa wa kufanya biashara kwenye Mabucha ambayo yanatarajiwa kukamilika Juni 15 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam machinjio imechelewa kuanza kutumika Kutokana na kutokamilika kwa Cold room, Mabucha ya Nyama, tank la maji, eneo la kuhifadhi mbolea, mageti na sehemu ya kuosha miguu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa