- Amtaka Mkandarasi kuongeza Kasi ya ujenzi.
- Mradi umeanza tangu mwaka 2019 lakini mpaka Sasa 2023 haujakamilika
- Mkandarasi anafanya mchezo wa kuleta mafundi siku akisikia Kuna ziara za Viongozi
- Serikali imemlipa Mkandarasi shilingi bilioni 7 kati ya 10 Lakini bado anasuasua.
- Wafanyabiashara walia Soko lao kuchelewa kuisha, Wanafanya biashara kwenye magumia
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameonyesha kukerwa na vitendo vya ubabaishaji wa Mkandarasi wa kampuni ya Namis Corporate Ltd anaejenga Soko la Tandale ambapo amemtaka kukamilisha ujenzi haraka.
RC Makalla ameshangazwa kuona mpaka sasa Mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 7 kati ya bilioni 10 lakini bado ujenzi unasuasua ambapo Kwa mujibu wa mkataba Soko likitakiwa kukamilika mwaka 2020 Kisha kuongezewa muda mpaka January 2023 lakini bado ameshindwa kukamilisha na anaomba kuongezewa miezi 6 Tena jambo ambalo Mkuu wa Mkoa amekataa.
Kutokana na changamoto hiyo, RC Makalla ameelekeza Halmashauri ya Kinondoni kumsimamia kikamilifu Mkandarasi na kuwaonya wasimpatie kazi nyingine kwenye Halmashauri hiyo.
Aidha RC Makalla amemtaka Mkandarasi kuongeza idadi ya mafundi na kuhakikisha kazi zinafanyika Kila siku Ili Soko likamilike.
Kwa upande wako Wafanyabiashara wa Soko Hilo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya Biashara kwenye mazingira magumu kutokana na uweze mdogo wa Mkandarasi.
Ujenzi wa soko la Tandale ulianza Rasmi September 14 mwaka 2019 na likitakiwa kukamilika September 2020 Lakini ilishindikana kukabidhi Kisha Kuongezewa muda mpaka January 2023 ambapo Leo Mkuu wa Mkoa amefika na kukuta Soko halijakamilika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa