-Atoa Siku 14 kwa LATRA, wamiliki wa mabasi na Jeshi la polisi kupitia muongozo ulioruhusu Uwepo wa Vituo binafsi vya Mabasi (Private Bus Terminal)
-Asema mfumo wa Kisasa wa udhibiti mapato kukamilika ndani ya wiki mbili
-Autaka Uongozi wa Stendi kurasimisha wadau wote wanaofanya shuguli Stendi ya Mbezi ili kudhibiti vibaka na watu wanaosumbua na kutapeli abiria
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Agosti 11,2022 amekutana na Kufanya Kikao na Uongozi wa Magufuli Bus Terminal pamoja na Wamiliki wa mabasi na wadau wengine wa usafirishaji wa kituo hicho kikao ambacho kimefanyika katika Ukumbi wa Stendi hiyo gorofa ya tatu Wilaya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
RC Makalla wakati wa kikao hicho alipata wasaa wa kusikiliza maoni ya Uongozi wa Stendi, wamiliki wa mabasi na wadau wengine kutokana na kero 5 zilizowasilishwa kwake
Ambazo ni mabasi kutoingia ndani yanashusha abilia nje,Uwepo wa Ofisi ya kutolea huduma nje ya Kituo kinyume na Serikali, Askari wa Suma JKT kushirikiana na wakatisha tiket kupitisha abiria bila tiketi,Kuwepo kwa wafanyabishara nje ya Kituo ambao sio rasmi,Uharibifu wa Mazingira kutokana na kuwepo kwa watu wasio na sifa ikiwemo vibaka
Aidha kupitia kikao hicho ilibainika kuwa kero hizo zipo ndipo RC Makalla akatoa Maelekezo yafuatayo
Mosi ametoa siku 14 kwa LATRA, wamiliki wa mabasi na Jeshi la polisi kupitia muongozo ulioruhusu Uwepo wa Vituo binafsi vya Mabasi kuanzia leo Agosti 11,2022.
Hata hivyo ameutaka Uongozi wa Stendi kurasimisha wadau wote wanaofanya shuguli Stendi ya Mbezi ili kudhibiti vibaka na watu wanaosumbua na kutapeli abiria wanaokuja kupata huduma.
Vilevile ili kudhibiti upotevu wa mapato katika Kituo hicho kikuu cha mabasi amesema ndani ya wiki mbili kuanzia leo Agosti 11, 2022 mfumo wa kieletroniki wa kudhibiti mapato utakuwa umekamilika.
RC Makalla amewahakikishia wananchi na watumiaji wa Stendi ya Magufuli Usalama na huduma bora, wanachotakiwa ni kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa