- Awasha pump kusukuma maji tanki la lita milioni 15
- Ameshukuru Rais samia kutoa fedha Bilioni 23 kukamilisha mradi lita milioni 70
- Aagiza kufikia Jumanne November 01 maji lita milioni 70 yafike mjini kupunguza mgao maji
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amewasha rasmi Pump ya kusukuma maji kutoka kwenye Visima vya Maji Kimbiji na Mpela kuelekea kwenye tank la kupokea na kusambaza maji Kigamboni na Katikati ya mji ambapo inatarajiwa kutoa huduma kwa Wananchi kuanzia Jumanne ya November 01.
Akizungumza wakati wa mwendelezo wa Ziara ya kukagua vyanzo vya Maji Kigamboni, RC Makalla amesema Mradi huo unakwenda kupunguza makali ya tatizo la mgao wa maji Kigamboni na katikati ya mji.
Aidha RC Makalla amesema visima hivyo vinazalisha Lita Milioni 450 kwa saa na maji yanayozalishwa yanapelekwa kwenye tank lenye uwezo wa kupokea Lita Milioni 15
Kutokana na uhitaji mkubwa wa maji uliopo, RC Makalla ameelekeza DAWASA kuhakikisha Mkandarasi anafanya kazi usiku na mchana ili ifikapo Jumanne Lita Milioni 70 ziwe zimefika kwa Wananchi.
Hata hivyo RC Makalla amesema tayari Serikali ya Rais Samia imefanikisha kupatikana kwa Mkandarasi wa Ujenzi wa Bwawa la Kidunda litakalokwenda kumaliza tatizo la mgao wa maji pindi mvua zitakapochelewa kunyesha na muda wowote kuanzia Sasa Serikali itasaini mkataba na Mkandarasi huyo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mpaka Sasa visima 7 Kati ya 12 vya Kimbiji na Mpela vimekamilika na vile ambavyo havijakamilika vipo hatua za mwisho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa