Mwonekano wa Mto Ngo'mbe Kinondoni- Dar es Salaam.
- Amtaka Mkandarasi kumaliza Mradi November mwaka huu.
- Amshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitiada zake za kufanikisha Mradi huo unaolenga kuondoa mafuriko Mto Ng'ombe na Kiboko.
- Mbunge Tarimba na Wananchi Wampongeza Rais Samia kwa kuwajali.
- Mradi ulisimama yangu mwezi January kwa madai ya malipo na Serikali umeshafanya Malipo ya Shilingi Bilioni 20 Kati ya Bilioni 30.
Ni Kufuatia Mkandarasi kuondoka site kabla ya kukamilisha Ujenzi.
- Mradi huo unajenga Barabara, vivuko 12 katika Kata 11 lengo likiwa ni kudhibiti mafuriko.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemtaka Mkandarasi kutoka Kampuni ya CHICO anaetekeleza Mradi wa Ujenzi wa Mto Ng'ombe Wenye urefu wa Km 8.5 kurudi eneo la kazi na kukamilisha kazi iliyobaki ili lengo la Serikali kumaliza Kero ya mafuriko kwa Wananchi ikamilike.
RC Makalla ametoa agizo Hilo wakati wa ziara ya kukagua Miradi huo na kukuta Mkandarasi hayuko eneo la kazi licha ya kulipwa zaidi ya Asilimia 60 ya Fedha.
Aidha RC Makalla amemuelekeza Mkandarasi kuongeza Nguvu kazi ili kazi iweze kukamilika na kukabidhiwa kabla ya November mwaka huu.
Kuhusu Wananchi waliolipwa fidia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 6 na bado hawajaondoka, RC Makalla ameelekeza wote waliolipwa kupisha Mkandarasi akamilishe kazi ambapo amesema atapita kila wiki kukagua maendeleo ya Ujenzi.
Hata hivyo RC Makalla amewataka TARURA kumsimamia Mkandarasi huyo aanze Ujenzi wa Barabara ya mtaa huo ikiwa ni Baada ya kupokea malalamiko ya Wananchi kuhusu ubovu wa Miundombinu ya Barabara hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa