-Aongoza makundi mbalimbali, Bodaboda, wanafunzi, Viongozi na watumishi wa Muhimbili kufanya usafi
- Ahamasisha Uchangiaji wa damu na Chanjo ya Uviko-19
Kufuatia Maadhimisho ya Sikukuu ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanzania Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla ameongoza makundi mbalimbali kufanya usafi katika hospitali ya Muhimbili huku wananchi wa maeneo mengine ya Mkoa huo wakifanya Usafi katika vituo vya Afya vya karibu yao.
RC Makalla akiongea baada ya zoezi hilo amesema Mkoa umeamua kuadhimisha Sikukuu ya Muungano kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za afya katika Mkoa ikiwa ni muendelezo wa Kampeni ya Usafi " SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM"
Aidha Mkuu wa Mkoa baada ya kupokea taarifa ya uchangiaji damu ambayo imekuwa ni 80% na inashuka hadi kufikia 50% amehamasisha uchangiaji wa damu kuwezesha kuwepo kwa akiba ya damu ili kuokoa maisha ya wahitaji
Sambamba na hilo RC Makalla amewataka wananchi kuchanja chanjo ya Uviko-19 kwa kuwa taarifa ambazo anapokea Ofisini kwake kila siku zinaonyesha Ugonjwa upo na ukifuatilia wengi wanaougua na kuwa katika hatari zaidi ni wale ambao hawajachanja, hivyo "Ujanja ni Kuchanja" Alisema RC Makalla
Baada ya zoezi hilo la usafi washiriki wameendelea kuchangia damu na kuchanja chanjo ya Uviko-19
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa