RC Makalla akikagua Maendeleo ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Kunduchi- Kinondoni
- Maeneo yaliyokuwa na changamoto ya Huduma ya Afya na Elimu Kinondoni sasa yapata Huduma hizo
- Awaomba wananchi husika kutoa Ushirikiano ili kazi ikamilike kwa wakati na kuitunza Miradi hiyo
-Ataka Migogoro ya Ardhi ya Nyakasangwe na Mabwepande ifike mwisho
-Kuhusu Mgogoro wa Barabara Salasala Buyuni- RC Makalla amewataka DC, My Fair, Opec kukutana ofisini kwake Alhamisi
-Kwa upande wa zoezi la Anuani za Makazi awapongeza Kinondoni na kutaka Halmashauri nyingine zifanye vizuri
-DC Kinondoni akiri kupokea na kutekeleza maelekezo yote sambamba na kusimamia Miradi hiyo ili pesa iendane na kazi husika
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 11 Aprili 2022 amefanya ziara katika Wilaya ya Kinondoni ili kujionea Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya
Akiwa Katika Wilaya hiyo RC Makalla amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Kuupiga mwingi katika utekelezaji wa Miradi hiyo ambapo zaidi ya Bilioni nane zimeelekezwa ili Kujenga Madarasa na Shule za Sekondari Dar es Salaam ikiwemo Kinondoni
Katika Ziara hiyo *Mkuu wa Mkoa* amejionea maeneo yaliyokuwa na changamoto ya Huduma ya Afya na Elimu Kinondoni sasa yamepata Huduma hiyo na kuwafanya wananchi kuendelea kuweka Imani kwa Serikali ya Awamu ya Sita
Aidha, RC Makalla amewaomba wananchi husika kutoa Ushirikiano kwa wakandarasi ili Miradi inayotekelezwa iweze kukamilika kwa wakati
Kuhusu Migogoro ya Ardhi ya Nyakasangwe na Mabwepande Mkuu wa Mkoa ametaka utekelezaji wa mapendekezo tume iliyoundwa kufanya kazi hiyo na kumaliza kazi yake
Hata hivyo katika Mgogoro wa Barabara ya Salasala Buyuni Mkuu wa Mkoa amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, My Fair, Opec na wajumbe husika kufika ofisini kwake siku ya alhamisi kulizungumzia suala Hilo huku wananchi wakipata njia ya kupita na Kuomba wananchi wawe watulivu na kutoa Ushirikiano ili Jambo hilo limalizike vema
Kwa upande wa Zoezi la Anuani za Makazi RC Makalla amewapongeza Wilaya ya Kinondoni kwa kufanya vizuri kiwilaya na kutaka Wilaya zingine kuongeza bidii sambamba na Kuifanya Ajenda ya Anuani za Makazi kuwa ajenda ya kila asubuhi kabla ya kufanya Jambo lolote
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe akiri kupokea maelekezo yote na kuahidi kuyafanyia kazi sambamba na kusimamia Miradi hiyo ya Maendeleo ili pesa iliyotengwa iendana na Mradi ( kazi) husika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa