- Awataka LATRA kutokwepa majukumu Na nyaraka zao walizotoa kwa stendi binafsi
- Aruhusu stendi binafsi 5 zilizohakikiwa Na LATRA kuendelea kutoa huduma Kwa sharti la kuingia na kutoka wapitie stendi Magufuli
- Aagiza Manispaa ya Ubungo kukaa Na wamiliki wa stendi binafsi kuona njia bora kukusanya mapato
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametangaza kuondoa katazo lililokuwa likizuia Mabasi yaendayo mikoani na nje ya Nchi kutoruhusiwa kupakia abiria au kushusha katika Vituo binafsi na badala yake ameruhusu utaratibu huo kuendelea Kwa sharti la kila basi kuingia ndani ya Kituo kikuu Cha Mabasi Cha Magufuli.
RC Makalla ametoa maamuzi hayo wakati wa kikao Cha pamoja baina ya LATRA, Wamiliki wa Stendi binafsi na Halmashauri ya Ubungo na kubaini pasipokuwa na shaka kuwa Waliotengeneza Vituo binafsi walifuata taratibu na kupatiwa Vibali na LATRA Baada ya kukidhi vigezo.
Miongoni mwa vigezo vilivyotolewa na LATRA ili kuruhusiwa kuanzisha Stendi binafsi ni pamoja na uwepo wa Vyoo, Sehemu ya mapumziko kwa abiria, viburudisho Na sehemu ya maegesho.
Kutokana na Hilo RC Makalla ameridhia Vituo binafsi 5 ambavyo ni Dar lax, ABC, Kilimanjaro, Shabiby, na Kimbinyiko vilivyohakikiwa kuendelea kutoa huduma na kufungua milango kwa wamiliki wengine wanaohitaji kuwa na Vituo binafsi kushirikiana na LATRA ili wapatiwe vigezo vinavyohitajika ambapo wamepewa Mamlaka ya kufuta au kutoa leseni.
Aidha RC Makalla ameagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukaa kikao Mara moja na wamiliki wa Stendi binafsi ili kuona njia Bora ya ukusanyaji wa mapato
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa