Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge amesema Ujenzi wa Stand mpya ya Mabasi ya mikoani ya Mbezi Louis umefikia 90% na itaanza majaribio ya Kwanza Novemba 25 na kuanza kutumika rasmi Novemba 30.
Kutokana na hilo RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye stend hiyo ikiwemo fremu za maduka, migahawa, ofisi, huduma za kifedha, supermarket, ofisi za kukata tiketi na hoteli ambapo zoezi la kutuma maombi limeanza leo Novemba 09 Hadi Novemba 25.
Aidha RC Kunenge amesema uwepo wa stand hiyo utaendelea kufungua fursa za maendeleo kwa Wakazi wa Ubungo hivyo amewataka kujiandaa kwa hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa