Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa onyo kwa Watu wote wanajihusisha na Wizi wa Magari, Vifaa vya Magari na Pikipiki ambapo amesema Vyombo vya usalama vinaendelea na operesheni ya kuwasaka wezi hao ambapo adi Sasa zaidi ya Watu 49 wanashikiliwa kwa wizi na ununuzi wa Vifaa vya wizi.
Akitoa Mrejesho wa Operesheni iliyoanza juzi, RC Kunenge amesema kupitia msako uliofanyika wamefanikiwa kukamata Vifaa mbalimbali ikiwemo Taa za magari, Side mirror, power windows, Bampa, Vioo, Gearbox, Radio, Rim na vifaa vingine vingi.
Kutokana na hilo RC Kunenge amesema kamwe hatoruhusu uhuni na Wizi wa namna hiyo kuendelea Katika Mkoa huo ambapo pia ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa wenzake kutokubali Vifaa vya wizi kuuzwa Katika Mikoa yao.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Kamishina Lazaro Mambosasa amesema miongoni mwa waliokamatwa ni Wauzaji wa Vifaa vya wizi ambao wamekuwa wakiwatuma wezi kwenda kuiba magari na vifaa.
Katika msako huo pia wamefanikiwa kukamata Gari iliyokuwa ikitumika kusafirisha Vifaa vya wizi pamoja na Pikipiki zilizoibiwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa