Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo March 03 amepokea Magari 20 na Kontena 65 za kuhifadhi taka zenye thamani ya Shilingi bilioni 4.1 ambapo amewahimiza wakazi wa Dar es salaam kuhakikisha wanazingatia suala la usafi wa mazingira.
Akipokea Magari hayo kwenye Bandari ya Dar es salaam, RC Kunenge ameyagawa kwa Halmashauri zote za Dar es salaam ambapo Halmashauri ya Jiji imepatiwa Magari 5, Manispaa ya Temeke Magari 8, Kinondoni Magari 5, Ubungo Gari 1 na Kigamboni Gari 1.
RC Kunenge amewaelekeza Wakurugenzi wa Manispaa zote kuhakikisha suala la usafi linapewa kipaombele huku akitaka magari hayo kutunzwa ili yadumu Muda mrefu na kutatua kero ya usafi.
Aidha RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi kuepuka tabia ya kutupa taka kwenye mitaro na mito kwani kwa kufanya hivyo wanasababisha mitaro kuziba huku akisema watakaohusika kuchafua mazingira Sheria itafuata mkondo.
Kwa upande wake Mratibu wa Miradi ya Bank ya Dunia chini ya TARURA na DMDP Humphrey Kanyenye amesema lengo la miradi wanayosimamia ni kuhakikisha wanaboresha mazingira ya Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira kuwa Safi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa