-Asema Serikali tayari imeshatoa zaidi ya bilioni 50 kwa ajili ya fidia
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Ofisini kwake Ilala Boma ambapo amesema bomoa bomoa inaendelea katika bonde la mto msimbazi ili kupisha uendelezaji wa kingo za mto msimbazi, na miundombinu mingine ya kisasa
Aidha RC Chalamila amesema kupitia uboreshaji wa mto msimbazi litapatikana eneo nzurii kwa ajili ya Shughuli za utalii na ujenzi wa hotel pembezoni mwa mto msimbazi hivyo wale wote ambao wameshalipwa fidia waende wakajenge katika maeneo mazuri wasiende tena kujenga mabondeni "ni vizuri kuchukua taadhari kwa kutojenga mabondeni kwa kuwa mvua bado zipo" Alisema RC Chalamila
Hata hivyo RC Chalamila amewataka viongozi wa Kata na mitaa kusimamia vema usafi katika maeneo yao ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
Mwisho RC Chalamila ametangaza tarehe ya ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi kwa Wilaya ya Kigamboni na Ilala kuanza tarehe 19/04/2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa