Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo wakati akishiriki mjadala wa ajenda ya Mwanaume katika malezi, Usawa wa Kijinsia, Afya, Elimu na Uchumi uliokuwa ukiendeshwa na Kituo cha EFM kupitia jukwaa la "MSHUA MASTA"
RC Chalamila amesema mwanaume aanze kuondoa dhana ya baadhi ya vitu ni vya mwanamke kwa mfano iko dhana kupika, kunyosha nguo, kufanya usafi nyumbani, kuosha vyombo ni kazi ya mwanamke tu hiyo sio sawa kila kinachofanywa na mwanamke kinaweza kufanywa na mwanaume pia Jamii iondokane na mifumo dume ili kujiletea maendeleo " ilifika wakati wanawake walikua wananyimwa hata fursa ya kusoma hili Sio sawa ebu fikiria sasaivi tuna Rais Mwanamke hivi mzazi wake angemnyima fursa ya kusoma ingekuaje? " Alisema RC Chalamila
Aidha RC Chalamila amewataka wanawake ili kwenda sawa, kile ambacho wanakitamani kwa mwanaume awe nacho, kuhakikisha na wao wanafanya juhudi za kuwa nacho, kwa kufanya hivyo itachagiza maendeleo katika Jamii.
Sambamba na hilo Mhe Chalamila alimekabidhiwa ngao maalum kwa ajili ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Philip Isdory Mpango kama kielelezo cha MSHUA MASTA, kwa kuwa mtu wa karibu anayeshirikiana na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.
Ifahamike kuwa MSHUA MASTA ni jukwaa maalum la kuongeza ushiriki wa wanaume Katika masuala ya kijinsia ili kuleta maendeleo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa