RC Chalamila akifurahia jambo na vijana wa machepe katika mto ulioko eneo la mabwepande mapema leo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo mapema leo alipotembelea mto Mabwepande ambako amekutana na kikundi cha vijana maarufu kwa jina la Mshikamano Group kinachojishughulisha na usafishaji wa mto pamoja na utunzaji wa mazingira, ikiwa ni muendelezo wa kutembelea maeneo yenye uwezekano wa kupata athari za mafuriko nyakati za mvua ambapo Mkoa uko katika maandalizi ya kujiweka sawa kukabiliana na mvua nyingi za El-Nino ambazo kwa mujibu wa TMA wametabiri uwezekano wa kunyesha mvua hizo hivi karibuni
RC Chalamila amesema vijana ni kundi kubwa wamekua wakijifanyia Shughuli halali za kujipatia kipato na dhamira ya Mhe Rais Dkt Samia ni kuweka mazingira rafiki kwa vijana kujipatia kipato hivyo kama kuna fursa katika usafishaji wa mito makundi yote mawili ya wakandarasi na vijana wa machepe wapewe fursa sawa " Ndio maana nasema simuogopi mtu yeyote ninamaana wala rushwa, wezi na wanao kandamiza maisha ya watu wa chini pia amewataka waandishi kutoposha habari kwa masilahi ya wala Rushwa'' Amesema RC Chalamila
Aidha RC Chalamila ametembelea eneo la Basihaya Tegeta ambalo hupata athari za mafuriko mara kwa mara hasa nyakati za mvua amemuagiza Mkuu wa Wilaya Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule kuunda timu ya wataalam ambao watapita eneo hilo kuona njia asili za maji kama zitakua zimezibibwa ziwekwe sawa ili kuzinusuru kaya zinazopatwa na athari za mafuriko.
RC Chalamila akiwa na wananchi wa Basihaya Tegeta akikagua eneo linalopata athari za mafuriko nyakati za mvua
Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa ametembelea ujenzi wa Shule ya Sekondari Changanyikeni kuona maendeleo ya ujenzi huo na kumtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati na kuzingatia thamani ya pesa.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amemuhakikishia mkuu wa Mkoa kuendelea kusimamia maagizo yake anayotoa na kutekeleza kwa wakati kwa masilahi mapana ya wana Kinondoni na Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Mwisho Mhe RC Chalamila akiwa Mabwepande aliambatana na wataalam mbalimbali kutoka NEMC, DAWASA, bonde na mratibu wa Kikosi kazi Mkoa Dkt Elizabeth Mshote, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Kamati ya Usalama ya Wilaya na wadau wengine wa Mazingira
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa