Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Februari 5,2024 wakati wa hafla ya Kusherekea mwaka mpya wa Jamhuri ya Muungano ya watu wa China katika Ofisi za ubalozi wa nchi hiyo Masaki-Kinondoni Jijini Dar es Salaam
RC Chalamila akiongea wakati wa hafla hiyo amesema urafiki wa nchi hizo mbili na wa kihistoria ambao uliasisiwa na Viongozi wa mwanzo wa mataifa hayo, kwa upande wa Tanzania Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere na China Hayati Mao Tse Tung ambapo viongozi wa nchi hizi mbili waliofuata katika awamu zote wameendeleza mahusiano na mashirikiano baina ya nchi hizo.
Aidha katika awamu hii chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetia fora kwa kuimarisha zaidi mahusiano na mashirikiano na Jamhuri ya Muungano ya watu wa china husani kupitia ziara ya Kitaifa aliyoifanya Novemba 2022 kufuatia mualiko wa Rais wa China Mhe Xi Jiping.
Hadi sasa ni ukweli usiopingika uhusiano wa Tanzania na China ni imara sana " Nafarijika kusema Dar es Salaam ni sehemu nzuri ambapo raia wengi wa China wanaishi na leo wawakilishi wa Jamhuri ya watu wa china imekusanyika hapa Kusherekea mwaka mpya 2024,
Napenda kutoa shukrani kwenu kwa mahusiano na mashirikiano ya muda mrefu ambayo yamekua na mchango mkubwa katika nyanja za kiuchumi na kijamii baina ya nchi hizi mbili" Alisema RC Chalamila.
Mwisho RC Chalamila aliwatakia heri ya mwaka mpya 2024
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa