Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Januari 26, 2024 katika hafla ya Siku ya Utamaduni (Cultural Day) iliyoandaliwa na chuo cha Taifa cha ulinzi Tanzania ( National Defense College- Tanzania) Kunduchi Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam
Akiwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro RC Chalamila amesema hakuna Taifa linaloweza kujidhihirisha mbele ya mataifa mengine Duniani kuwa ni Taifa hai kama halina Utamaduni " Niwaombe kila mmoja apende na ajivunia Utamaduni wake" Alisisitiza RC Chalamila
Aidha RC Chalamila amefurahishwa na Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania NDC ambacho kinatoa mafunzo kwa mataifa mbalimbali Duniani hususani nchi za Afrika kuweka katika kalenda ya kitaaluma siku ya Utamaduni ambapo mataifa mbalimbali hupata fursa ya kuonyesha tamaduni za nchi zao hivyo kudhihirisha uhai na umuhimu wa tamaduni pia kuibua fursa adhimu za kujifunza tamaduni za mataifa mengine.
Sambamba na hilo RC Chalamila alipata wasaa wa kujionea tamaduni za mataifa mbalimbali takribani 16 yakionesha tamaduni zao ikiwemo vyakula mbalimbali, mavazi na mifumo mbalimbali ya starehe za mataifa hayo na kusisitiza lugha kama kigezo mojawapo cha Utamaduni kitumike katika Mawasiliano na Maarifa.
Kwa upande wa Mkuu wa NDC Meja Jenerali WA Ibuge amesema siku ya Utamaduni ni sehemu ya mafunzo kwa Taifa linalokuja kupata mafunzo ya Katika chuo hicho na ipo katika kalenda ya kitaaluma, hufanyika kila mwaka ambapo mwaka huu mataifa 16 ambayo ni Burundi, Botswana, Egypt, Ethiopia, India Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda, Sierra Leone,South Africa, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania yameonesha tamaduni zao
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa