Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila leo Novemba 7, 2023 ameyasema hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa juu ya utumwa na utumwa wa kisasa (mambo leo) katika historia ya kisasa ya Afrika uliofanyia katika Ukumbi wa chuo kikuu cha Dar es salaam.
Aidha RC Chalamila amesema hali ya biashara ya utumwa iliyopita bado mifumo yake ina athari kwenye maisha tuliyonayo sasa kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi, hali inayokosesha uhuru kwa jamii husika.
Mhe. Chalamila alisema, "Bado kuna mabinti ambao si tu wanasafirishwa kwenda nje ya nchi bali husafirishwa kutoka mikoani kuja DSM na wakati fulani kufichwa kwenye baadhi ya nyumba na kufanyishwa kazi ambazo si sahihi, na kama mlivyoona sisi tumeanza na kampeni muhimu sana ya kuona suala hilo tunalikomesha katika mkoa wetu."
Vilevile RC aliongezea kwamba katika mkutano huo kutajadiliwa kwa upana zaidi na kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika kutatolewa elimu kwa mbinu za kitaalum za kukomesha biashara hizo haramu zikiwemo na zile za kuwapeleka mabinti nchi nyingine za Afrika na hata nje ya Afrika
Kwa upende wa Salvatory Nyanto ambaye ni Mhadhiri mwandamizi idara ya Historia naye alisema kupitia mkutano huo mkubwa wa kimataifa umeweza kuwavutia watafiti, wanafunzi, wanazuoni, wanaharakati kutoka nchini Urusi, Ulaya na Marekani na baadhi ya nchi za Afrika kujadili maisha baada ya utumwa na hali ya sasa na kutoa mapendekezo kwa tafiti zilizopo na namna gani yakukomesha kabisa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa