Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amesema TASAF imekua mkombozi mkubwa wa kuondoa umasikini katika Jamii watu wengi wamebadili maisha yao, pia ni ukweli usiopingika kati ya programu nyingi zilizoanzishwa kwa lengo la kupunguza umasikini miongoni mwa jamii TASAF ni ya mfano.Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo mapema leo Dsemba 22, 2023 katika kikao cha tathmini cha utekelezaji mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila alisema TASAF imekuwa msaada mkubwa sana katika kuboresha kaya maskini kwenye nyanja anuai kama vile huduma za elimu, afya na kuinua watu kiuchumi hivyo TASAF inatakiwa kuwafikia walengwa wengi zaidi waliokusudiwa.
Pia RC Chalamila amewaasa waratibu na wataalam wengine wa TASAF kuwajengea utambuzi wanufaika wao kwa kuwa pesa hazikamilishi maisha ya mwananadamu na kuna wengine wanatakiwa kunufaika, "Kama mtoto atapata ajira, akaajiriwa halafu akaruhusu mzazi wake aendelee kuwa kwenye TASAF maana yake kijana huyo anahitaji viboko mbele ya mzazi wake."Vilevile RC Chalamila alisema kuna muhimu kwa wanafaika wahusishwe katika vikao kama hivyo ili wapate kujua kinachoendelea na aliwahimiza viongozi wawe na nidhamu za kiutumishi na pesa zinazotolewa zipelekwe kwa walengwa hayo ndio matarajio ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu na sio vinginevyo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa