Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila aliyasema hayo leo Novemba 21,2023 wakati akifungua rasmi soko la Zakhem lililopo kata ya Kibonde Maji Mbagala.
Mhe.Chalamila alisema yeye ni mtu anayenda ukweli na kuchukia ubabaishaji ambapo hapo awali hilo soko lilitekwa na madalali wanaowanyonya wafanyabiashara na wajariamali wanyonge.
RC Chalamila alisema, "Nilitoa onyo kwamba tujirekebishe wote, uroho wakutamani kila mali hautatufikisha popote kwahiyo sisi kama watumishi wa umma lazima tujenge kiasi ili kila mmoja aweze kunufaika na keki ya taifa."
Aliongezea, "Viongozi waliotuteua tukifanya vitu vya ovyo na watumishi wenzetu, wananchi wanamchukia raisi aliyetuteua sisi, tukifanya matendo mema, matendo ya huruma na matendo yanayogusa watu sifa nzuri zinaenda kwa raisi wetu." Na alitoa rai kwa viongozi kuifanya Mbagala kuwa ya miradi mikubwa kwakuwa ndiyo mlango wa mikoa ya kusini ili waweze kukusanya mapato kwa maendeleo zaidi.
Pia RC alitoa pole kwa wote waliokumbwa na athari za mvua hizi za El-Nino ila alitilia mkazo wakazi waliojenga mabondeni kiholela wahame na walinde watoto kuzuia maafa ya maji, kuachana na biashara za laana ikiwemo madanguro.
Naye mkuu wa wilaya ya Temeke mhe Sixtus Mapunda amesema soko hilo ni chanzo cha mapato na mifumo ya sasa imeangalia waasisi wa mwanzo wa soko, watu wa vipato vya chini na wanyonge wapate sehemu.
Kwa upande wa mbunge wa jimbo hilo la Mbagala mhe Abdallah Chaurembo alitumia nafasi hiyo kumshukuru mhe raisi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazotoa kwa kuboresha maendeleo kwa sekta za barabara, afya na elimu.
Soko hilo lililogharimu Tsh bilioni 2.48 lilikaguliwa na kufunguliwa na RC Chalamila Agust 8, 2023 likiwa limekamilka kila kitu cha miundo mbinu lakini watu wa hali ya chini walikuwa wamebaguliwa na kunyimwa haki zao.RC CHALAMILA SOKO LIANZE, MADALALI KAENI PEMBENI.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila aliyasema hayo leo Novemba 21,2023 wakati akifungua rasmi soko la Zakhem lililopo kata ya Kibonde Maji Mbagala.
Mhe.Chalamila alisema yeye ni mtu anayenda ukweli na kuchukia ubabaishaji ambapo hapo awali hilo soko lilitekwa na madalali wanaowanyonya wafanyabiashara na wajariamali wanyonge.
RC Chalamila alisema, "Nilitoa onyo kwamba tujirekebishe wote, uroho wakutamani kila mali hautatufikisha popote kwahiyo sisi kama watumishi wa umma lazima tujenge kiasi ili kila mmoja aweze kunufaika na keki ya taifa."
Aliongezea, "Viongozi waliotuteua tukifanya vitu vya ovyo na watumishi wenzetu, wananchi wanamchukia raisi aliyetuteua sisi, tukifanya matendo mema, matendo ya huruma na matendo yanayogusa watu sifa nzuri zinaenda kwa raisi wetu." Na alitoa rai kwa viongozi kuifanya Mbagala kuwa ya miradi mikubwa kwakuwa ndiyo mlango wa mikoa ya kusini ili waweze kukusanya mapato kwa maendeleo zaidi.
Pia RC alitoa pole kwa wote waliokumbwa na athari za mvua hizi za El-Nino ila alitilia mkazo wakazi waliojenga mabondeni kiholela wahame na walinde watoto kuzuia maafa ya maji, kuachana na biashara za laana ikiwemo madanguro.
Naye mkuu wa wilaya ya Temeke mhe Sixtus Mapunda amesema soko hilo ni chanzo cha mapato na mifumo ya sasa imeangalia waasisi wa mwanzo wa soko, watu wa vipato vya chini na wanyonge wapate sehemu.
Kwa upande wa mbunge wa jimbo hilo la Mbagala mhe Abdallah Chaurembo alitumia nafasi hiyo kumshukuru mhe raisi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazotoa kwa kuboresha maendeleo kwa sekta za barabara, afya na elimu.
Soko hilo lililogharimu Tsh bilioni 2.48 lilikaguliwa na kufunguliwa na RC Chalamila Agust 8, 2023 likiwa limekamilka kila kitu cha miundo mbinu lakini watu wa hali ya chini walikuwa wamebaguliwa na kunyimwa haki zao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa