Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Oktoba 20,2023 Ofisi kwake Ilala Boma wakati akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu maboresho ya Shirika la Masoko Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila amewataka wananchi kuepuka matapeli wanaowalaghai kutoa pesa ili kuwapatia eneo la Biashara katika Soko hilo Jipya, ambapo amesema maendeleo ya ujenzi wa Soko hilo kwa sasa umefikia asilimia 91, Soko likikamilika litakuwa na maduka 2055 awali kabla ya kuungua moto Soko hili lilikuwa na maduka 1662.
Aidha RC Chalamila amesema Soko likikamilika Mkoa utalikabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia kwa ajili ya Uzinduzi kisha litakabithiwa Shirika la Masoko Kariakoo ambapo taratibu zingine zitafuata kwa Uwazi lakini wale wote waliohakikiwa awali watapewa kipaumbele na kupatiwa ridhaa ya kupanga kwa mujibu wa sheria.
Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa ameleza maboresho yatakayofanyika katika katika Soko hilo ikiwemo uendeshaji wa kidigitali, kufunga taa na kamera, Kuimarisha ulinzi na Usalama ili biashara zifanyike saa 24
Sambamba na hilo Mhe Chalamila amesema ameunda kamati ya zaidi ya watu 15 kwa ajili ya maboresho ya Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC) kwa lengo la kuhuisha zaidi Shirika hilo liwe na tija kwa masilahi mapana ya Umma.
Mwisho Rais Mhe Dkt Samia Suluhu dhamira yake ni kuona masoko na mashirika yanakuwa na tija ndio maana ameendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika Soko la Kariakoo tayari ameshatoa pesa Bilioni 28.03 kukamilisha ujenzi huo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa