Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amesema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili (TATAKI) kwa masilahi mapana ya Taifa la Tanzania.
RC Chalamila amesema hayo leo Julai 04, 2023 katika Ukumbi wa Maktaba Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam akiwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani (MASIKIDU 2023) ambayo yameshirikisha wadau wa Kiswahili kutoka nchi mbalimbali Duniani, na mwaka huu kilele kitakuwa Julai 7, 2023 Zanzibar
Mhe Albert Chalamila amesema huwezi kutenganisha Kiswahili na Utamaduni wa Mtanzania, hivyo Serikali wakati wote itaendelea kushikamana bega kwa bega na TATAKI katika juhudi za kuendeleza lugha hiyo katika dhana ya maendeleo endelevu
Aidha amesema Lugha ya Kiswahili imekuwa ikitumika kitaaluma na Kimawasiliano hata hivyo katika nyakati za sasa lugha hiyo imekuwa ikipitia Changamoto katika kukua kwake kutokana na uvamizi wa lugha zingine nchini, hivyo hatupaswi kukaa kimyaa lazima tuendelee kupiga kelele katika matumizi ya lugha hiyo kwa ufasaha katika nyanja mbalimbali ndani na nje ya nchi, bahati nzuri Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ana utashi mkubwa na lugha ya Kiswahili
Kwa Upande wa Prof. Bernadeta Killian wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam amesema Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili imekuwa na mipango mikakati mingi katika kukuza lugha ya Kiswahili ikiwemo mkakati wa Kushirikiana na wadau, Ufadhiri wa Kusoma Kiswahili kwa mataifa mbalimbali nchini, vilevile Punguzo la Ada
Mwisho RC Chalamila alipata wasaa wa kuzindua machapisho na kugawa vyeti kwa wadau mbalimbali wa lugha ya Kiswahili
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa