Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Novemba 18, 2023 wakati wa Kongamano lililoandaliwa na Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) katika Ukumbi wa Hotel ya Hyatt Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila akiwa katika Kongamano hilo alipata wasaa wa kujionea bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na Wanawake wajasiriamali wa kitanzania hususani Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kwa takribani miaka mingi Wanawake walikosa nafasi za kuonyesha ubunifu na uwezo wao kutokana na mfumo dume "Iko mijadala ya kitaalam ambayo inaonyesha dhahiri mwanamke ni Smart sana mfano mzuri chunguza kwa makini uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan, mwanamke akijitambua ni mkombozi kwa familia, jamii na Taifa kwa Ujumla" Alisema RC Chalamila
Aidha RC Chalamila amebainisha namna Rais Dkt Samia Suluhu anavyo weka mazingira rafiki ya kibiashara hususani kwa wajasiriamali kuwaunganisha na masoko ikiwemo uboreshaji wa miundombinu, Ununuzi wa Ndege ya Mizigo na hata uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kufungua fursa za uwekezaji.
Vilevile amewataka Wanawake wote kutumia kongamano hilo kujadili na kujenga uelewa wa ujasiriamali na masoko na kuendelea kuhamasisha Wanawake wengi zaidi kutumia fursa za kijasiriamali kwa maendeleo endelevu.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Bi Mwajuma Hamza amesema kongamano hilo linawakutanisha Wanawake wajasiriamali kujadili na kujenga uelewa wa ujasiriamali na masoko ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa masilahi mapana ya jamii na Taifa kwa Ujumla.
Vilevile TWCC imemuomba Mhe Mkuu wa Mkoa kupeleka Salamu kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele kuwwzesha Wanawake kwa kuwapatia mitaji,kuwashirikisha katika sera na uboreshaji wa miundombinu unayosadifu ujasiriamali
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa