-Amshukuru Rais Dkt Samia kwa kuwa kinara katika kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji
-Asema uwekezaji unatoa fursa za ajira na kukuza uchumi.
Hayo yamejiri jana Oktoba 19, 2024 wakati akizindua magari ya kisasa yanayotengenezwa na kampuni ya Kifaru Motors aina ya GWM Tank 500 HEV - Golden Tulip Hotel Masaki
RC Chalamila alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji wa ndani na nje ambapo makampuni mbali mbali ikiwemo yanayounganisha magari yanakuja kuwekeza katika nchi yetu hususani Mkoa wa Dar es Salaam.
Hiyo ni fursa kubwa na yakipekee ambayo inawezesha vijana wengi wa kitanzania kupata ajira ambazo zinawawezesha kujikimu kimaisha na kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Aidha RC Chalamila alisema magari hayo ni mazuri sana, yanamuonekano mzuri pia yametengezwa kisasa zaidi hivyo wananchi wanunue magari hayo.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Kifaru Motors Brig Gen Michael Luwongo alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa uzinduzi wa magari hayo ambapo alisema GWM Tank 500 HEV ni gari ya kwanza inayotumia umeme kuanzishwa hapa Tanzania
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa