Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameahidi kujiridhisha na uhalali wa kuwepo kwa vituo vidogo vidogo vya mabasi katika Jiji la Dar es Salaam ambavyo hupelekea mabasi ya abiria yaendayo Mikoani kutopita kushusha na kupakia abilia katika Stendi kuu ya mabasi "Magufuli Bus Terminal" Mbezi mwisho
RC Chalamila amefikia hatua hiyo kufuatia malalamiko yaliyotolewa na wadau, wajasiriamali na wafanyabishara wanaofanya biashara katika kituo cha mabasi yaendayo Mikoani Magufuli, wakati alipotembelea kituo hicho na kupata wasaa wa kusikiliza kero zao.
Aidha miongoni mwa malalamiko yaliyotolewa ni Stendi hiyo kutokukusanya mapato ipasavyo, wafanyabishara kutokufanya biashara vizuri ambapo kuna uwezekano mkubwa kufikia hatua ya kushindwa kulipa Kodi kwa wale waliopanga fremu katika Stendi hiyo.
Kwa upande wa Wafanyabishara wadogo nao wamesema wanakosa wateja kwa kuwa magari mengi yanayoenda mikoani hayapiti kushusha abilia wala kupakia kitendo ambacho kinasababisha kuwepo kwa idadi ndogo ya watu.
Hivyo RC Chalamila amesema stendi ya Magufuli imejengwa kwa gharama kubwa lazima hatua za haraka zichukuliwe kunisuru stendi hiyo ili iwe na tija
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa