- Azitaka Halmashauri za Manispaa kutumia vizuri Kitengo cha Mkaguzi wa ndani na Kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila kwa nyakati tofauti akiwa katika kikao cha Baraza maalum la kupitia hoja za mdhibiti na mkaguzi wa Hesabu za Serikali* (CAG) katika Manispaa ya Ubungo na Kinondoni amezitaka Halmashauri hizo kuwa na mikakati ya kuzuia hoja za CAG na sio kujibu hoja hizo.
RC Chalamila amezipongeza Manispaa hizo kwa kupata hati safi katika Kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 kufuatia ripoti ya CAG ambapo licha ya kuwa na hati safi bado kuna maeneo CAG amebainisha mapungufu (hoja) ziko hoja amabazo zimeshafungwa na zingine ziko katika hatua za Utekelezaji.
Aidha kwa muktadha huo RC Chalamila ameelekeza juhudi kubwa iwekwe katika kuzuia hoja zisitokee na sio kujipanga kujibu, hivyo amewataka kuhakikisha zoezi la ukaguzi linakuwa endelevu, vilevile kila Halmashauri ijengee uwezo kitengo cha mkaguzi wa ndani na kukitumia vizuri Kitengo hicho.
Hata hivyo RC Chalamila amewataka kujibu kwa wakati hoja za CAG, Utekelezaji wa maagizo ya LAAC, kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wanaoisababishia Halmashauri hoja na kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato na kudhibiti upotevu wa fedha za umma
Sambamba na hilo Barabaza la Madiwani lisimamie mienendo ya ovyo katika Halmashauri na kumsaidia Mkurugenzi katika Utekelezaji wa majukumu yake kwa masilahi mapana ya Umma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa