Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Novemba 24,2023 wakati akifunga maonesho ya majukwaa ya mitaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ngazi ya mitaa yaliyofanyika viwanja vya Biafra ya Kinondoni.
RC Chalamila amesema kupitia majukwaa kutawafanya wanawake wajasiriamali wafike mbali zaidi kiuchumi na wawe majasiri kwakuwa mwanamke akiwa na uchumi mzuri anajiamini pia ni chachu katika maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla.
"Kama mlivyokuja hapa leo kuwezesha jambo hili, kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe anatoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha majukwaa haya yanakuwa na tija kubwa kwenu na kwa jamii ya watanzania. Msiishie tu kuyaunda na kusema tuna majukwaa 127," alisisitiza kwa wadau hao.
Vilevile Mhe Chalamila aliwatia moyo wajasiriamali waliohudhuria waendelee kupambana na kwamba mwanamke akishika rungu la kiuchumi familia nyingi zinapona a hivyo kila mwanamke afanye kazi zake.
Pia RC Chalamila alimshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Muwasisi wa majukwaa haya kwa kuboresha miundo mbinu ya kibiashara kwa akina mama ambapo amekuwa kiongozi wa kuigwa na ameuthibitishia ulimwengu kuwa hakuna linaloshindikana.
Naye mwenyekiti Taifa wa majukwaa ya uwezeshaji Wanawake kiuchumi Bi. Fatuma Kange alitoa shukrani zake kwa Mhe Rais kwa fursa mbalimbali anazowapa huku akiahidi kushirikiana na wadau ili malengo yatimie na wafike mbali zaidi, vilevile waliomba kuanzishwe SACCOS ya wilaya ili waepukane na mikopo kausha damu na aliwasihi wajariamali kutumia kitandao ya kijamii kwa faida ikiwemo kutangaza bidhaa zao.
Baadhi ya wadau hao ni pamoja na CRDB, DCB, Azani, TRA, Brela, Polisi Dawati Jinsia na Watoto, Bunju Women Empowerment, NMB, Huduma za Afya Kinondoni, Hapa Kazi tu, Vijimambo, Makongo Juu, Tam Tam, Nguzo Yetu, Neema Chai na wengineo wakiwa majukumu ya kuanzisha, kuendesha na kusimamia huku kauli mbiu ikiwa ni 'Uwezeshaji wanawake kiuchumi familia imara uchumi imara, kazi iendelee.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa