Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo mapema leo Julai 8, 2023 wakati akiongoza matembezi maalum kuanzia Mlimani City- Mwenge ITV na kuhitimisha tena viwanja vya Mlimani City, maarufu kwa jina la "Bima Walk" yenye lengo la kukuza uelewa kwa jamii kuhusu Bima, ambayo yameandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)
RC Chalamila ametaka hamasa zaidi na elimu kuhusu Bima itolewe kwa jamii ili wananchi wafahamu umuhimu na faida ya Bima lakini pia mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania kuja na ubunifu wa kuwa na vifurushi ambavyo vitakuwa rafiki kwa watu wa kipato cha chini.
Aidha Mhe Chalamila ameelekeza matembezi mengine ya aina hiyo yafanyike katika maeneo yenye watu wengi kama Karikaoo, na Mbagala, vilevile amesistiza Viongozi wenye mamlaka mbalimbali kuwa mstari wa mbele kukata Bima kwa kuwa Bima ziko za aina mbalimbali mfano Bima ya Afya, Elimu, na Usalama wa biashara.
Kwa Upande wa Kamishna wa TIRA Dkt Baghayo Saqware amesema Mamlaka imeaandaa matembezi hayo ambayo yanafaida kiafya kwa kuwa mazoezi ni Afya lakini lengo kubwa ni kuelimisha na kuhamasisha jamii umuhimu na maana ya Bima, kwa kuwa Bima inakinga dhidi ya majanga
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa