Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 5, 2023 ametangaza Kampeni kubwa ya siku 10 ya upimaji Afya bila malipo kwa wakazi wa Wilaya zote 5 za Mkoa huo.
Akiongea na Waandishi wa Habari RC Chalamila amesema Uzinduzi rasmi wa Kampeni hiyo kimkoa utafanyika katika viwanja vya Zakhiem Mbagala katika Manispaa ya Temeke siku ya jumatatu Julai 10, 2023 na baada ya hapo upimaji wa Afya utaendelea katika kila Wilaya zote za Mkoa huo na Kampeni itaendelea hadi Julai 19,2023
Aidha Mhe Chalamila amesema Kampeni hii kubwa itahusisha Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Saratani Ocean Road, Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali za Mkoa na watoa huduma kutoka Halmashauri na Hospital kubwa zinazomilikiwa na Taasisi binafsi na wadau wengine wa Afya.
Wakazi wa DSM watapata fursa ya kupima Afya zao hasa magonjwa yasiyoambukiza amabayo yamekua yakiwaathiri Watanzania wengi pia wakazi watahamasishwa kujenga utamaduni wa kupima Afya zao wale watakao bainika na matatizo ya kiafya watapatiwa huduma za Rufaa.
Vilevile RC Chalamila amesema huduma zitakazo tolewa ni kuanzia ngazi ya Huduma ya Afya ya msingi, kibingwa, na kibobezi katika nyanja za Uchunguzi wa Saratani mbalimbali, Magonjwa ya Moyo shinikizo la damu na huduma ya uchangiaji damu kwa hiari, chanjo dhidi ya Uviko 19, chanjo ya watoto chini ya miaka 5.
Kwa Upande wa Manga Mkuu wa Mkoa Dkt Rashid Mfaume ametoa ratiba ya zoezi hilo katika Halmashauri ambapo *Manispaa ya Temeke Julai 10 na 11, 2023 Viwanja vya Zakhiem Mbagala, Manispaa ya Kigamboni 12 na 13, 2023 Viwanja vya Mjimwema, Manispaa ya Ubungo Julai14 na 15 2023 Viwanja vya Barafu Manispaa ya Kinondoni Julai 16 na17 Tanganyika Peckers Kawe na kuhitimisha Jiji la Dar es Salaam Julai 18 na 19 katika Viwanja vya Mnazimmoja
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa