Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila, Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Molel leo Agosti 17, 2024 wameshiriki matembezi ya kuhamasisha kuchangia ujenzi wa wodi ya mama na mtoto pamoja na ukarabati wa majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila akiongea baada ya matembezi hayo ambayo yalianzia fukwe za Coco hadi viwanja vya Karimjee amesema Rais Dkt Samia amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya katika nyanja za vifaa tiba, majengo na wataalam hivyo Mkoa kwa kutambua juhudi za Mhe Rais umeamua kuunga Mkono kwa kuhamasisha jamii hususani marafiki wa Amana kuchangia ujenzi wa wodi ya mama na mtoto na ukarabati wa majengo mengine ya kutoa huduma katika Hospitali hiyo, ambapo zaidi ya Bilioni 3 zinahitajika.
Aidha kwa upande wa Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Molel ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema Rais Dkt Samia Suluhu kutokana na uwekezaji wake katika sekta ya Afya amefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya mama na mtoto hivyo amepongeza hatua inayofanywa na Mkoa kupitia Hospitali ya Amana ambapo amewahakikishia wizara iko pamoja nao kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea.
Sanjari na hilo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dkt Bryceson Kiwelu amesema kihistoria hospitali hiyo ni ya miaka mingi hadi sasa ina takribani miaka 70 ni hospitali pekee ndani ya Wilaya ya Ilala inayohudumia idadi kubwa ya watoto ndiyo maana wamekuja na wazo la kujenga wodi ya kisasa na kufanya ukarabati wa baadhi ya majengo ili kuwezesha huduma bora ya mama na mtoto hiyo matembezi hayo ni moja ya sehemu ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha ambazo zitawezesha utekelezaji wa mradi huo ambao unatija kubwa kwa jamii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa