- Awataka Wazazi Kuchangia Chakula cha watoto shuleni
-Asema Mhe Rais Dkt Samia ameendelea kuboresha miundo mbinu ya Shule ni jukumu la kila mtu kuhamasisha watoto kwenda shule
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi katika shule ya Msingi Vijibweni na Kisiwani ambako alipata wasaa wa *kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo ambayo inajengwa vyumba vya madarasa sita kwa ufadhiri wa fedha za BOOST
Akiwa katika shule hizo amemtaka mjenzi kukamilisha maeneo yote ambayo bado, ili vyumba hivyo vya madarasa vianze kutumika kwa ajili ya kujifunzia na kufundishia.
RC Chalamila amesema watoto wasipopatiwa Chakula shuleni ni vigumu kufanya vizuri katika masomo yao hivyo uchangiaji wa chakula mashuleni sio jambo la hiari ni lazima kwa mzazi mwenye mtoto kuchangia
Aidha RC Chalamila amesema Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kuboresha miundo mbinu ya Shule kwa kiasi kikubwa hivyo jukumu la kila mmoja ni kuhamasisha watoto kwenda shule pasiwe na watoto wasiondikishwa kwenda shule wakati wanasifa ya kuanza Shule.
Vilevile ameutaka uongozi wa Wilaya hiyo kusimamia *miradi ikamilike kwa wakati, kutatua kero za wananchi hususani migogoro ya Ardhi na kuendelea kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Halima Bulembo amuomba Mkuu wa Mkoa kupeleka salamu za shukrani kwa mhe Rais Dkt Samia kwa namna anavyotoa fedha zinazotekeleza miradi mingi ya maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwemo miradi ya barabara kupitia DMDP
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa