Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila Januari 27,2024 amezindua wiki ya sheria katika Mkoa huo iliyopambwa na maandamano kutoka mahakama ya kisutu hadi viwanja vya Mnazimmoja
RC Chalamila akiongea wakati wa ufunguzi wa wiki ya sheria ametoa rai kwa wakazi wa Mkoa huo kutembelea mabanda ya maonesho ya wiki ya sheria ili kupata elimu na ushauri wa kisheria na kutoa mapendekezo yatakayo saidia kuongeza umakini na ubora katika mhimili wa utoaji haki.
Aidha maadhimisho hayo ya wiki ya sheria yaliyobeba kauli mbiu " Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa: nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha mfumo Jumuishi wa Haki Jinai" ambapo RC Chalamila amesema kauli mbiu hiyo inagusa maeneo yote muhimu ikiwemo umuhimu wa kushirikisha wadau katika myororo mzima wa utoaji haki.
Vilevile RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika mhimili huo muhimu wa utoaji haki uwekezaji huo unajidhihirisha katokana na matumizi ya teknolojia ya TEHAMA na uteuzi wa majaji ambao amekuwa akiufanya hususani majaji Wanawake hivyo kurahisisha utendaji wa Shughuli za Mahakama.
Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mhe Salma Maghimbi amesema wiki ya sheria ni kiashiria cha kuanza kwa shughuli za sheria kwa mwaka mpya 2024 hivyo wiki hii ya sheria inatoa fursa kwa wananchi kuja kujifunza majukumu ya mahakama hapa nchini vilevile kupata elimu na ushauri wa kisheria kupitia mabanda ya maonesho yaliyoko katika viwanja hivi hadi Kilele cha siku ya Sheria Februari 1, 2024 hivyo niendelee kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazimmoja
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa