Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amezindua rasmi Kampeni kabambe ya kupima Afya bila malipo kwa wakazi wa Mkoa huo katika viwanja vya Zakhiem Mbagala, Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa Uzinduzi huo ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupima Afya mara kwa mara huku akiainisha huduma za Uchunguzi wa Afya ambazo zitatolewa kupitia Kampeni hiyo ikiwemo Uchunguzi wa Saratani za aina mbalimbali, magonjwa ya macho, Afya ya Kinywa na meno, magonjwa ya ngozi, Magonjwa ya Moyo, shinikizo la damu, Tezi dume, magonjwa ya kina mama na watoto, Kisukari, chanjo dhidi ya UVIKO-19 na Chanjo ya watoto chini ya umri wa miaka 5, na magonjwa mengine mengi ya kuambukiza na yasiyoambukiza, pamoja na uchangiaji wa damu
RC Chalamila amehamasisha wanchi kukata bima ya Afya ambayo itawasaidia kupata matibabu katika nyakati ambazo wanakua hawana pesa taslimu kwa kufanya hivyo ni rahisi kuokoa maisha pindi unapougua ghafla na hauna pesa za matibabu, hata hivyo Mhe Chalamila amewataka Viongozi na jamii kuheshimu taaluma ya Udakitali kutokana na mchango wao mkubwa kwa ustawi wa jamii.
Aidha RC Chalamila amekemea mtindo wa kuwa na imani za kwenda kwa waganga wa kienyeji pindi unapougua badala ya kwenda hospital kupata vipimo vya kisayansi, pia amezishukuru Taasisi za afya zote zinaoshirikiana na Mkoa katika Kampeni ya kupima Afya bila malipo.
Kwa Upande wa mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Rashid Mfaume amesema wananchi kutumia fursa hiyo ya kupanda vipimo bila malipo lakini pia kujenga tabia ya kupima Afya mara kwa mara kwa kuwa unaweza kujiona uko sawa kumbe unatatizo ambalo ungundua mapema kutibu ingekua ni rahisi.
Mwisho zoezi la Upimaji Afya katika Mkoa limezinduliwa leo Julai 10,2023 na linatarajiwa kuwafikia wananchi zaidi ya elfu 20 ambapo kwa Wilaya ya Temeke wananchi wataendelea kupata huduma hadi Julai 11, 2023, Kigamboni Viwanja vya Mjimwema Julai 12-13, 2023, Ubungo Julai 14-15, 2023 Viwanja vya Barafu, Kinondoni 16-17, 2023 Viwanja vya Tanganyika Peckers Kawe na Jiji la Dar es Salaam 18-19 Viwanja vya Mnazimmoja
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa