-Mradi huo utatekezwa katika Mikoa miwili Dar es Salaam na Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 3, 2024 amezindua mradi wa kuimarisha huduma za Ukunga kwa niaba ya Waziri wa OR-TAMISEMI hafla ambayo imefanyika katika Kituo cha Afya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila amemshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma za afya hapa nchini hususani huduma za afya ya uzazi na mtoto ambapo tunashuhudia kupungua kwa vifo vya akina mama waja wazito kwa kiasi kikubwa
Aidha RC Chalamila amesema Mkoa huo takribani kina mama 160,000 hujifungua kila mwaka hivyo basi watoa huduma wenye ujuzi na weledi wanatakiwa kuwepo ili akina mama wapate huduma stahiki kulingana na viwango vya kitaifa na kimataifa.
Vilevile RC Chalamila amesema juhudi hizo za Serikali zimekuwa zikiungwa mkono na wadau wa Afya katika kufadhiri Mafunzo kwa watumishi, na kununua vifaa tiba ambapo wenzetu UFDPA, AMREF na TAMA kupitia ubalozi wa Canada wamedhamilia kushirikiana na Serikali katika kutekeleza mradi unaolenga kutoa huduma ya Afya ya uzazi na kuboresha huduma za Ukunga Tanzania.
Kwa Mkoa wa Dar es Salaam mradi utatekezwa katika Wilaya 3 Temeke, Kinondoni na Ilala, mradi unategemewa kugharimu jumla Dola ya Canada 11,750,000 sawa na TZS 22,085,065,000. ambapo mradi utawafikia akina mama waja wazito 1,071852 wakina mama watakao jifungua pamoja na watoto wachanga 805,945, zahanati 180, vituo vya afya 28 na hospitali 12 kata 28 na vijiji 112 vitafikiwa na mradi huu
Mwisho mradi utasaidia kuongeza idadi ya wauguzi wakunga, kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi, kuboresha ujuzi na weledi kwa wakunga na kuzuia masuala mtambuka kama kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi, huduma rafiki kwa vijana na huduma za uzazi wa mpango kwa wasiofikiwa na huduma hizo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa