Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 12, 2023 amezindua mpango wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga kwa Kuimarisha mfumo wa usafirishaji wa dharula kwa wajawazito na watoto wachanga maarufu kwa jina la M-MAMA.
RC Chalamila akizindua mpango huo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa dhamira yake ya kutokomeza kabisa vifo vya kina mama na watoto wachanga vinavyotokana na uzazi ambapo amewataka wadau na hata watumishi wa umma kuunga mkono mpango wa M-MAMA ili kuleta ustawi na kukuza uchumi wa Taifa, tayari ameshaelekeza mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani kutekeleza mpango wa Kidigitali wa M-MAMA.
Aidha Mhe Chalamila amesema mpango mkakati wa maradi ni kuondoa ucheleweshaji unaoweza kutokea Katika ngazi tatu zinazopelekea wanawake wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga kupata madhara yatokanayo na uzazi na wakati mwingine kupoteza maisha, ucheleweshaji huweza kutokea Katika kufanya maamuzi, kutafuta huduma, usafiri wa kufikia huduma na ucheleweshaji wa kupata huduma zilizo bora
Kwa upande wa mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Rashid Mfaume amesema lengo la Mkoa ni kuondoa kabisa vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga kwa Kuimarisha maeneo matatu ambayo ndiyo yameonekana kuwa ni Changamoto kubwa eneo la ucheleweshaji wa kufanya maamuzi ya kutafuta huduma, usafiri kufikia huduma na kupata huduma zilizo bora.
Mwisho hafla ya Uzinduzi huo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Anatouglo Mnazimmoja na kuhudhuriwa na watalaam wa Afya kutoka OR-TAMISEMI, Sekretarieti ya Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Mameya, na waganga wa kuu wa Wilaya, Wataalam wa Afya na wadau wengine wa M- MAMA kama Vodacom.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa