Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 28,2023 amezindua uwasilishaji wa matokeo ya Sensa 2022 huku akiwataka Watendaji wa Kata, mitaa, na Wenyeviti wa Manispaa za Mkoa huo kuhakikisha wanafikisha taarifa za matokeo ya Sensa ya watu na Makazi kwa wananchi pamoja na kuwaelimisha namna ya kuzitumia taarifa hizo, katika kuongeza kasi ya maendeleo.
Aidha RC Chalamila amesema matumizi sahihi ya takwimu hizo ni muhimu kwa ustawi wa jamii katika mkoa huo ambao unaidadi kubwa ya watu kuliko mikoa mingine ya Tanzania, kwa kuwa mataifa yaliyopiga hatua za kimaendeleo Duniani hutumia data za Sensa katika kupanga maendeleo na kuwa na sera zinazolingana na kile kinachopatikana kutokana na Takwimu za Sensa.
Mafunzo hayo ya uwasilishaji wa matokeo ya Sensa ya watu na Makazi 2022 kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kueleza matumizi sahihi ya matokeo hayo ni mafunzo ya awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza ilifanyika machi 14, 2023
Hata hivyo kwa upande wa Mwakilishi wa mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi Fausta Mtigiti amesema utekelezaji wa mpango kazi wa Usambazaji mafunzo hayo ni chimbuko la matokeo ya kitaifa ambayo yalizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan yakihusisha ngazi za kiutawala
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa