Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 27 amezindua kitalu cha miti katika Ofisi za Bonde la Mto Wami, Ruvu zilizoko Ubungo Maji Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila amepongeza menejimenti ya bonde na wadau wa mazingira katika Mkoa huo kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika masuala yanayohusu mazingira pia wataalam wa Bonde Mto Wami,Ruvu Ofisi ya Dar es Salaam kwa wazo la kuwa na kitalu cha miti chenye miche takribani elfu 55. "Nchi yetu na Dunia kwa ujumla inapitia Kipindi cha mabadiliko ya tabia ya nchi lazima uwekezaji mkubwa ufanyike kukabiliana na janga hilo hivyo Kinachofanyika hapa ni mwanzo mzuri." Alisema RC Chalamila
Aidha RC Chalamila amesema mazingira yakitunzwa vizuri maji yanapatikana kwa wingi ambayo hutumika majumbani, viwandani, na hata kuzalisha umeme na vingine vinavyofanana na hivyo, ambapo amewataka wote waliokusanyika katika hafla hiyo wakiwemo makandarasi wa usafirishaji mito na vikundi vya machepe kuwa Kielelezo kizuri katika kupanda miti katika mito ili kuzuia ummonyoko wa Kingo za mito vilevile Taasisi kupanda miti rafiki kwa maji na miti ya matunda katika maeneo yao.
Sambamba na hilo RC Chalamila amezitaka Taasisi, Mamlaka na Mashirika pamoja na Halmashauri zote za Mkoa kuja na mawazo ya kibunifu ya kuboresha mazingira hususani "Road Reserve" zilizoko katika Mkoa huo
Kwa upande wa Bi Hadija Faraji Afisa Bonde wa Bonde Mto Wami/Ruvu Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam amesema kitalu kilichozinduliwa leo kina jumla ya miti ya aina mbalimbali ambayo ni rafiki wa maji na matunda takribani elfu 55 na wanategemea kuongeza hadi kufikia laki moja kwa lengo la kuwafikia watu wengi zaidi.
Mwisho Mhe Albert Chalamila amegawa miti kwa wadau mbalimbali wa mazingira waliohudhuria hafla hiyo na kuwataka kupanda miti hiyo na kuendelea kuwa mabalozi wazuri katika utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Ifahamike kuwa moja ya majukumu ya mamlaka ya Bonde la Mto Wami Ruvu ni kufanya ufuatiliaji na tathimini za rasimali maji moja ya utekelezaji wake ni kupanda miti rafiki wa maji kwa lengo la kutunza vyanzo vya maji
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa