Vivo Energy Tanzania, kampuni inayosambaza vilainishi vya Shell na Engen, imezindua rasmi kampeni yake mpya kabisa, ‘Shell Tumerudi Kivingine Kata Kilomita’, inayolenga kurudisha upya vilainishi vya Shell katika soko la Tanzania.
Mhe Chalamila amezindua kampeni hii Leo Oktoba 7,2024 akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Viongozi pamoja na watumishi wa kampuni katika makao makuu ya kampuni hiyo Masaki jijini humo.
Mhe Chalamila ameipongeza kampuni hiyo akibainisha kuwa kampeni hii inalingana na malengo ya maendeleo ya Taifa. “Serikali ya Tanzania imeweka mazingira wezeshi kwa biashara kustawi, hasa katika sekta ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa viwanda na maendeleo ya kiuchumi ya taifa letu, Kurudishwa kwa vilainishi vya ubora wa juu vya Shell kwenye soko letu ni hatua kubwa mbele katika kuchangia dira yetu ya 2025 ya ukuaji endelevu wa uchumi,” alisema Chalamila
Vilevile Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy Tanzania, Bw.Mohamed Bougriba, alisema kuwa kampeni hii ni ishara ya kujitolea kwa kampuni hiyo kutoa bidhaa bora na huduma bora kwa wateja wake. “Tunafurahi kuwapa wateja wetu vilainishi vya Shell kwa namna inayowapa ubora, uaminifu, na ubunifu wa chapa hii ya Kimataifa,” alisema Bougriba.
Kwa upande wa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vivo Energy Tanzania, Aileen Meena, alieleza kuwa kampeni hii inalenga kuwawezesha watanzania kuboresha maisha yao ya kila siku kwa kutumia bidhaa za ubora wa juu pia kampeni hii itawawezesha watanzania kubadilisha shughuli zao za kila siku kwa kutumia bidhaa za utendaji wa hali ya juu na ushirikiano endelevu, imara, unaoweza kuleta maendeleo kwa miaka mingi ijayo.
Aidha, RC Chalamila amewahimiza vijana kuchangamkia fursa zinazotokana na kampeni hii, akisisitiza kuwa itaongeza ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Mwisho, kampeni ya ‘Shell Tumerudi Kivingine Kata Kilomita’ itafanyika katika vituo vyote vya huduma vya Engen Nchini, na itatoa fursa kwa wateja kupata bidhaa za Shell kwa bei nafuu na kupata zawadi mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa