Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Mei 23, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa JNICC wakati wa utambulisho wa program ya Imarisha Uchumi na Samia (IMASA)
RC Chalamila amesema programu hiyo inalenga kuwawezesha wananchi wa Tanzania bara na Visiwani ambayo itakuwa na madhumuni yafuatayo, kupata takwimu za wananchi waliopo kwenye maeneo husika na shughuli zao katika maeneo hayo, kupata mahitaji ya kiuchumi kwenye maeneo husika kwa kushirikiana na viongoziwa wilaya na Mkoa, kujenga uwezo wa wananchi wote wenye uhitaji kwenye maeneo husika, kutekeleza programu ya kuwezesha wananchi kwenye mikoa na maeneo yao
Aidha RC Chalamila amesema pamoja na kwamba Serikali inafanya jitihada mbalimbali za kuwawezesha wanawake kiuchumi bado ni vema kila mmoja akatumia changamoto anazopitia kuwa fursa “ Wako wengi ambao wamepitia changamoto nyingi hawakukata tamaa walichukulia kama fursa na leo wanamafanikio makubwa” Alisema RC Chalamila
Sanjari na hilo programu inayotambulika kama Imarisha Uchumi na Samia (IMASA) ni sehemu ya Jitihada za uwezeshaji wanawake na makundi maalum kwa mikoa yote 31 ya Tanzania Bara na Visiwani programu hii ni kwa kipindi cha miezi sita kuanzia januari 2024 hadi julai 2024 itahusisha wanufaika 62,000 ambapo baraza la uwezeshaji wanawake kiuchumi ndiye msimamizi mkuu wa programu hii kwa kushirikiana na ofisi za wakuu wa Mikoa,Wilaya, Wakurugenzi wa Manispaa, Majiji, Halimshauri za Wilaya na wadau wa maendeleo katika sekta husika Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu imedhamilia kuwezesha wananchi kiuchumi hususani wanawake Mwisho utambulisho wa programu ya IMASA umehudhuriwa na mamia ya wanawake wa Mkoa huo, Mkurugenzi mtendaji wa NEEC, Mshauri wa Rais masuala ya wanawake na Mkundi maalum Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Mpogolo na wadau wengine
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa