Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila ameyasema hayo leo Juni 1, 2023 wakati amekutana na Viongozi na watumishi wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke kwa nyakati tofauti ikiwa ni muendelezo wa Kujitambulisha toka apangiwe kuhudumu katika Mkoa huo.Akiongea na watumishi hao amewataka viongozi wa wilaya na Halmashauri kusimamia kwa weledi na kuzingatia thamani ya fedha wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu za manunuzi ya Umma.
Aidha RC Chalamila katika kikao hicho ametoa rai kwa Wah. Madiwani kuwa mstari wa mbele katika usimamizi wa miradi huku akiwataka kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Sambamba na hilo Mhe Chalamila ametoa rai kwa viongozi Idara ya Elimu kuja na mpango mkakati utakaosaidia kuinua elimu ndani ya wilaya hizo huku akilenga kuongeza mapato kwani uwezekano wa kufanya hivyo upo ikiwa tu wataamua kuwa wabunifu.
Akizungumzia suala la ukusanyaji wa mapato Mhe Mkuu wa Mkoa amesema kumekua na ukusanyaji usioridhisha hasa wa ushuru wa huduma ( Service Levy) hivyo ameelekeza watendaji kujipanga vizuri ili kusaidia katika ukusanyaji wa kodi hiyo.
Pia RC Chalamila akiwa Temeke alipata wasaa wa kukutana na Wazee wa Wilaya hiyo ambapo Wazee walionyesha kufurahishwa namna Mhe Chalamila anavyotekeleza majukumu yake siku chache toka alipo hamishiwa na Mhe Rais kuhudumu katika Mkoa huo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa