- Asema ulinzi na usalama, miundombinu ya barabara, maji, umeme, Afya, elimu, uwekezaji, viwanda na biashara kuendelea kupewa kipaumbele.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 28, 2024 amewasilisha utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi-CCM kwa Halmashauri Kuu ya Chama Mkoa mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM Ndg Abbas Mtemvu katika Ukumbi wa Manispaa ya Temeke Iddy Nyundo.
Akiwasilisha utekelezaji wa Ilani hiyo RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambazo zinatimiza ahadi ya CCM kwa wananchi iliyotolewa wakati wa uchaguzi na kutatua kero za wananchi na kuleta ustawi wa jamii.
RC Chalamila ameeleza bayana hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa ambapo amesema hali ni shwari na jitihada za kudhibiti vitendo vya kihalifu zinaendelea pamoja na kufanya Operesheni mbalimbali za kukabiliana na matukio ya kihalifu.
Aidha RC Chalamila amesema uwekezaji mkubwa umefanyika katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya Mkoa una jumla ya vituo vya Afya 1,436, vituo vya Serikali 190 na 1,246 vituo binafsi, Elimu Shule za msingi 953 za Serikali 415 na Binafsi 538 pia Shule za Sekondari ziko 368 ambapo 188 za Serikali na 180 ni binafsi
Vilevile kwa upande wa barabara kupitia TARURA inahudumia barabara zenye urefu wa Km 5,057.765 zenye lami ni Km 612.410, changarawe Km 1,641.601 na udongo Km 2,832.622.
Pia kupitia DMDP II Mkoa umepangiwa kuboresha zaidi ya Km 250 za Barabara katika Wilaya zote tano kwa gharama ya shilingi bilioni 988 vilevile kupitia TANROAD inahudumia mtandao wa barabara zenye Km 619.84 ikiwa Barabara Kuu Km 119.97 barabara za Mkoa Km 400.75 na zilizokasimiwa ni Km 99.12
RC Chalamila amesema ni ukweli usiopingika fedha ni nyingi katika Mkoa huo na miradi ya maendeleo ni mingi pia ikiwemo ya maji, uwekezaji , viwanda na Biashara, uchumi na uzalishaji na miradi mingine ikiwemo ya makundi maalum kama kuwezesha wazee
Mwisho Mkoa wa Dar es Salaam unaishikuru sana Serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na mwenyekiti wa CCM Taifa chenye Ilani ya kuleta maendeleo na ustawi wa maisha ya wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa