Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 11, 2023 ameongoza wafanyakazi wa Benki ya CRDB, wabia wa Benki ya CRDB Marathon, na Jogging club za Mkoa huo kufanya mazoezi kuanzia CRDB HQ hadi Green ground
Akiongea baada ya matembezi na mazoezi hayo RC Chalamila amewataka washiriki na wananchi wa Mkoa huo kutumia Benki ya CRDB kuhakikisha wanafungua akaunti na kufanya miamala, kukisajili kwa wingi CRDB Marathon na kushiriki, kwa kuwa Benki hiyo imekuwa ikitumia mapato yanayopatikana katokana na Marathon kuboresha miundo mbinu ya Afya na kuwahudumia wanawake na watoto hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua uchumi na ustawi wa jamii
Aidha Mhe Chalamila ameeleza umuhimu wa kufanya mazoezi ikiwa ni njia moja wapo ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza amabayo kwa siku za hivi karibuni yamekuwa yakiwaathiri watu wengi, lakini pia ni vizuri kuwa na bima ya Afya.
Sambamba na hilo kwa upande wa mtendaji mkuu wa Benki ya CRDB Ndg Abdulmajid Nsekela amesema Benki hiyo imekua ikiandaa matembezi hayo mara kadhaa na fedha zinazopatikana hupeleka kuboresha huduma za Afya kwa mfano tayari pesa hizo zimewezesha kufanyika kwa upasuaji wa watoto wadogo wenye matatizo ya moyo, Kujenga kituo cha Mawasiliano Ocean Road, na kuwasaiadia akina mama na watoto CCBRT hususani akina mama wenye matatizo ya fistula.
Vilevile kupitia Marathon ya Sasa wamepanga kukusanya zaidi ya Bilioni 2, kwa kuwa Benki hiyo inathamini mambo ya Muungano inatarajia kwenda kujenga Kituo cha Afya Zanzibar
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa