RC Albert Chalamila leo Octoba 2, 2023 ametembelea eneo lililokumbwa na ajali ya moto Kariakoo na kuzungumza na wafanyabishara ambapo amesema tayari ameshaunda kamati ndogo ndani ya siku saba itakuja na majibu ya sakata zima la Janga la moto uliotokea mapema Jumapili ya Octoba 1, 2023 ambao umeteketeza jengo na baadhi ya bidhaa za wafanyabishara.
RC Chalamila amewataka wale wote walioziba vipenyo au njia kati ya jengo moja na lingine kwa mujibu wa mipango miji kubomoa pia ametoa rai kwa wafanyabishara kukata bima ambayo itawanusuru pale majanga yanapotokea vilevile amewataka wadau wa bima kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabishara hao
Aidha RC Chalamila amewasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wafanyabishara wote wa Kariakoo hususani walifikwa na janga hilo la moto na kuwaomba kuendelea kuwa watulivu pia amevitaka vyombo vya habari kuepuka upotoshwaji kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi kutoka kwenye vyanzo sahihi
Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa alipata wasaa wa kusikiliza maoni ya wafanyabishara na kuwahakikishia Serikali na wadau wengine wa biashara wako karibu nao wawe na imani na Serikali.
Mwisho Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward mpogolo ameishukuru vyombo vya ulinzi na Usalama na Taasisi zingine binafsi ambavyo vilishiriki kikamilifu kuzuia kuenea kwa moto huo amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kujipanga vizuri dhidi ya majanga hayo ili yasitokee tena
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa